ANGALIZO
Huduma hii ni bure hivyo kuna matangazo katika Website hii
Ukibonyeza ikafunguka kusikotakiwa bonyeza Back ili urudi hapa
Ikiwa ni link unataka kufungua basi rudia kubonyeza tena itakupeleka sehemu sahihi
Katika makala iliyopita nimekuelekeza jinsi ya kupakuwa application ya Bing na Kujisajili
KAMA HAUJAISOMA
👇Soma Hapa👇
Bing Chat/Copilot ni huduma ya kipekee inayokuwezesha kuwasiliana na Bing Search kwa njia ya mazungumzo.
Unaweza kuuliza maswali, kupata majibu, kujifunza mambo mapya na hata kuomba Bing Chat/Copilot kukusaidia kutoa au kuboresha maudhui mbalimbali, kama vile mashairi, hadithi, nambari, muhtasari na zaidi.
Lakini je, unajua kwamba unaweza pia kutengeneza picha na Bing Chat/Copilot kwenye application ya simu?
Ndio, ni kweli.
Bing Chat/Copilot ina uwezo wa kuchora au kuunda picha za ubunifu kulingana na maelezo yako.
Unaweza kuomba Bing Chat/Copilot kukuchorea kitu chochote unachotaka, isipokuwa picha yako mwenyewe au zenye maudhui ya kiutu uzima.

Katika makala hii, nitakuonyesha jinsi ya kutumia Bing Chat/Copilot kwenye app ya simu kutengeneza picha za kuvutia.
Kabla tuendelee naomba nikudokeze, Bing wamefanya maboresho hivyo ile Chat imebadilishwa inaitwa Copilot hivyo mimi nitaandika vyote ili ukikuta Chat au Copilot usichanganye.
Sasa fuata hatua hizi rahisi:
Hivyo ndivyo unavyoweza kutengeneza picha na Bing Chat au Copilot kwenye app ya simu.
- Fungua app ya Bing kwenye simu yako ambayo nilikwisha kukuelekeza jinsi ya kuipata na kujisajili katika makala iliyopita(SOMA HAPA), kisha bonyeza "Chat au Copilot" kwenye menyu.
- Andika ujumbe wako kwa Bing Chat/Copilot ukitaja unataka kutengeneza picha.
Kwa mfano, unaweza kuandika "Tengeneza picha ya mtoto wa kitanzania akikimbizwa na mama yake, mkononi ameshikiria bakuri la wali kando ya nyumba duni" au "Tengeneza picha ya kijana wa kitanzania akiwa na mpenzi wake kando ya gari zuri".
ZINGATIA
Ili Bing akupe picha nzuri zaidi mpe malekezo ya Kiingereza.
Kwa uchunguzi wangu nimebaini maneno ya KiSwahili yanamsumbua kutoa matokeo mazuri
Bora hata Kiswanglish(yaani kuchanganya maneno).
Hivyo chukua maneno yako kisha rudi kwenye Bing Translator(ipo kwenye Home) na paste hapo au andika upya.
Usisahau kubadili lugha maana naona anaanza na Spanish, badili kwenda English.
Unaweza tumia Google Translate(nje ya application hii).
Ukimaliza kuandika bonyeza copy maneno yako ya Kiingereza kisha paste kwenye uwanja wa kuandikia maneno na kisha bonyeza Send. - Utaona maneno yanasomeka ⬛Stop Responding yakitoweka basi picha itaanza kutengenezwa.
- Subiri kama dakika 1 au 2 uone picha iliyotengenezwa na Bing Chat/Copilot.
- Zitatokea picha nne ambazo zinaendana na ulichoomba hivyo chagua itakayokuvutia
Picha zitaonekana kwenye skrini yako kama sehemu ya mazungumzo yako na Bing Chat/Copilot.
Kama katika picha zote ilizokupa hakuna iliyokuvutia unaweza kukopi yale maneno ya mwanzo na kuyaweka tena, rudia rudia mpaka ikupe picha unayotaka. - Furahia picha yako na uisambaze kwa marafiki zako ikiwa unataka.
Unaweza pia kuomba Bing Chat/Copilot kukufanyia marekebisho au mabadiliko kwenye picha yako kwa kuandika maoni yako.
Hivyo ndivyo unavyoweza kutengeneza picha na Bing Chat au Copilot kwenye app ya simu.
Ni rahisi sana na ni njia nzuri ya kuongeza ubunifu wako na kujifurahisha.
Picha zote unazoona katika post hii na ile ya maelekezo ya kwanza nimetumia Bing AI nikaambatanisha na screenshot za simu yangu
Jaribu nawewe uone matokeo yake.
TENGENEZA PICHA UNITUMIE ILI NIHAKIKI KAMA DARASA UMELIELEWA
IKIWA UTAPATA UGUMU WOWOTE BASI NIJULISHE
Tuma Picha na Wasiliana Nami Kwa: