Unaweza kuinstall na kutumia Bing kwenye simu za Android na iOS kwa kufuata hatua hizi rahisi:
- Fungua Google Play Store kwenye simu yako ya Android au App Store kwenye iOS kisha tafuta Bing.
- Chagua Bing kutoka kwenye orodha ya programu na bofya Install/Get.
- Subiri mpaka application imalize kuingia kwenye simu yako kisha bonyeza Open ili kuifungua.
- Ukibonyeza Open itaanza na logo ya Bing kama salamu kisha itafunguka na kukusubiri ubonyeze 'Continue to ask me everything' kisha subiri ili muanze mazungumzo kati yako na Bing Chat.
- Bing inakulazimu kujisajili kwanza kabla ikusaidie majibu au kutengeneza picha.
- Bonyeza Allow ambayo itatokea kwenye skirini yako ili kuruhusu Bing kufuatilia eneo ulilopo.
- Shuka chini kidogo utaona Sign in, hii imeelezea kabisa kwamba, ili uulize maswali mengi na muwe na mazungumzo marefu inakubidi kujisajili.
ZINGATIA HAYA
Wakiomba email, kwakuwa ni mara ya kwanza basi gusa Create One ili uanzishe akaunti ya Microsoft.Hapo weka email yako ya Google kwa usahihi, kama unayo nyingine unaweza kuweka ilimradi iwe na uwezo wa kupokea ujumbe, watatuma code kwenye email yako, zichukue na ujaze kukamilisha usajili.
Baada ya hapo wataomba password, majina yako, nchi uliyopo pamoja na tarehe/mwezi/mwaka wako wa kuzaliwa, ukimaliza hapa watakuwa wameshakutumia code kwenye email hivyo zijaze katika hatua inayofuata.Kwa sababu zilizo nje ya uwezo, ujumbe unaweza kutotoa taarifa hivyo fungua Gmail yako kisha angalia kwenye Inbox, ukikosa hapo kagua kwenye Spam/Junk.
ZIADA
Mwisho kabisa wanaweza kukutaka uthibitishe kuwa wewe sio roboti hivyo fuata maelekezo wanayokuuliza kwa usahihi na ukimaliza hapo tayari utakuwa umemaliza usajili - Sasa unaweza kutumia Bing kama kutafuta vitu mtandaoni, kuuliza maswali na kutengeneza picha kwenye simu yako.Unaweza kuandika au kuongea swali lako kwenye sanduku la utafutaji au kutumia ikoni ya kamera au msimbo wa QR ili kutafuta picha au bidhaa.
- Bing itakupa matokeo yenye ubora na ufanisi, pamoja na viungo(links), picha, video, ramani, habari na zaidi.
Unaweza pia kutumia vipengele vya ziada vya Bing, kama vile Bing Rewards, Bing Translator, Bing Wallpaper na Bing News.
Jaribu leo na uone tofauti!
KAMA UTAKUTANA NA CHANGAMOTO YEYOTE WASILIANA NAMI ILI TUITATUE
Wasiliana Nami Kwa: